Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 24 Desemba, 2016 amewasili mkoani Singida na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa huo  Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Singida.


Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, kesho tarehe 25 Desemba 2016 wanatarajia kuungana na waumini wengine wa dini ya Kikristo nchini  katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi mkoani Singida.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaomba waumini wa dini ya kikristo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi  kuungana na Rais Magufuli katika ibada ya Krismasi kwani imekuwa ni heshima kwao kutokana na uwepo wa  Rais Mkoani hapa kwa ajili ya sikukuu ya Krimass.

Dkt. Nchimbi amewataka wananchi wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais Magufuli na familia yake ili aendelee kuwatumikia watanzania katika kuwaletea maendeleo.


Amesema ni bahati kubwa kwa mkoa wa Singida kwa mara nyingine tena kumpokea Kiongozi huyo Mkuu wa nchi kwa kuwa katika kipindi kifupi mkoa huo pia ulimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipohudhuria sherehe za Maulidi.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Singida
24 Desemba, 2016

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: