Rais John Magufuli ameomboleza kifo cha mkuu wa mkoa mstaafu, Joel Bendera kilichotokea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). 


β€œJioni hii nimepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mkuu wa Mkoa mstaafu Dk Joel Nkaya Bendera, natoa pole kwa familia yake na wote walioguswa na msiba huu, pia naungana nao katika kipindi hiki cha majonzi,” amesema Rais Magufuli katika taarifa iliyotolewa na Ikulu leo Jumatano Desemba 6,2017.

Bendera amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Muhimbili alikofikishwa kwa ajili ya kupata matibabu.

Rais Magufuli amesema Bendera atakumbukwa kwa mchango alioutoa kwa Taifa akiwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo ukuu wa mkoa, naibu waziri na mbunge. Pia, katika maendeleo ya michezo.

β€œAlikuwa kiongozi shupavu, mahiri na mchapakazi, alipenda kufanya kazi kwa ushirikiano na daima alitamani kupata mafanikio makubwa katika majukumu aliyokuwa nayo, hakika tutamkumbuka,” amesema Rais Magufuli.

Pia, amewapa pole wananchi wa mikoa ya Manyara alikokuwa mkuu wa mkoa Oktoba 26,2017 na mkoani Tanga alikokuwa mbunge.

Rais Magufuli ametoa pole kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanamichezo na wote walioguswa na msiba huo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: