
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MWENYEKITI mpya wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage
amesema atafanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa na kwa kufuata sheria,
kanuni na Katiba ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam jana , Jaji Kaijage ambaye
uteuzi wake ulitangazwa jana na Ikulu, alisema taasisi anayoenda
kuifanyia kazi inaendeshwa kwa sheria za uchaguzi na katiba ya nchi.
“Kwa kweli niahidi utendaji unaozingatia sheria na katiba ya nchi,
nitafuata sheria, taratibu na kanuni zinazoongoza Tume ya Uchaguzi,”
alisema Jaji Kaijage, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani Tanzania.
Ataiongoza NEC kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Desemba 20, mwaka huu.
Jaji Kaijage alitoa msimamo huo baada ya gazeti hili kumuuliza namna
gani ataitumikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo imekuwa inalalamikiwa
na baadhi ya vyama vya siasa kuwa haiko huru kutokana na watendaji wake
kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama tawala.
“Hakuna namna nyingine ya kumpata mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kwa
sasa hivi, lazima katiba iongoze anapatikanaje, sio kwa sababu
nataeuliwa na Rais kwamba nitapindisha taratibu, hapana, nitafuata
sheria na katiba,” alisisitiza Jaji Kaijange, ambaye hata hivyo hakutaka
kuingia kwa undani, kwa maelezo kuwa hajaapishwa kushika wadhifa huo.
Uteuzi wa Jaji Kaijage ambao umefanywa na Rais John Magufuli,
ulitangazwa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Jaji
Kaijage amekuwa Mwenyekiti wa NEC akichukua nafasi ya Jaji mstaafu
Damian Lubuva, ambaye muda wake wa kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo,
umemalizika hivi karibuni.
“Jaji Semistocles Kaijage anachukua nafasi ya Jaji mstaafu Damian
Lubuva ambaye muda wake wa kuwa Mwenyekiti umemalizika rasmi mnamo
tarehe 19 Desemba 2016,” alieleza Balozi Kijazi katika taarifa yake
hiyo, iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Dar es
Salaam. Wasifu wake Jaji Kaijage alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa,
wadhifa alioushikilia kuanzia mwaka 2012.
Alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu kuanzia mwaka 2000 ambapo amewahi kuwa
Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Dodoma (2004-2006, Iringa (2006-2007) na Dar
es Salaam (2007-2012).
Kabla ya hapo, alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu mwaka 1988-89.
Wakati huo pia alikuwa mkuu wa mafunzo wa idara ya mahakama. Amewahi
kuwa Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa mwaka 1990-1992.
Kabla ya hapo, Jaji Kaijage amewahi kuwa Hakimu wa mahakama
mbalimbali nchini; na alipanda kuwa Jaji wakati huo akiwa Hakimu Mkuu
Mkazi.
Alisoma kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule ya Sekondari ya
Bihawana mkoani Dodoma mwaka 1970-1973; na baadaye alijiunga na kidato
cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Mkwawa, Iringa mwaka 1974
hadi 1975.
Mwaka 1979 -1982 alisoma Shahada ya Kwanza ya Sheria katika Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada yake ya Uzamili alisomea Chuo cha
Cardiff cha Chuo Kikuu cha Wales, Uingereza.
Uteuzi mwingine
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua tena Jaji mstaafu Hamid
Mahamoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC kwa kipindi kingine cha
miaka mitano kuanzia juzi, Desemba 20, mwaka huu.
Jaji Hamid alikuwa katika nafasi hiyo, kabla ya uteuzi huo kwa miaka
mitano. Muda wake kuwa katika nafasi hiyo ulikwisha Desemba 19, mwaka
huu.
Halikadhalika, Rais Magufuli pia amemteua Jaji mstaafu wa Mahakama ya
Rufaa, Jaji Harold Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia
Desemba 20, mwaka huu.
“Jaji mstaafu Nsekela anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji
mstaafu Salome Kaganda ambaye amestaafu mnamo tarehe 10 Desemba, 2016,”
ilieleza taarifa hiyo jana.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: