Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Khamis Mgeja amewaomba Watanzania kumsamehe waziri mkuu wa zamani,
Edward Lowassa kwa kushindwa kuwashukuru baada ya uchaguzi mkuu.
Ametaka wajue kuwa kada
huyo aliyehamia Chadema baada ya kukatwa jina lake kwenye orodha ya wagombea
urais wa CCM, sasa yupo kwenye kifungo cha kisiasa kutokana na Serikali kuzuia
mikutano ya hadhara.
Mgeja alitoa kauli hiyo
jana katika Kata ya Tumbi Manispaa ya Tabora wakati alipokuwa akiongea na
wanachama na viongozi mbalimbali wa Chadema, pamoja na wananchi wachache waliovamia
kikao.
Mgeja alisema anasikitishwa na kitendo cha Lowassa kuzuiwa kuwashukuru wananchi waliompigia kura kupitia mikutano ya hadhara na bado anaamini kuwa hawakumtendea haki.
“Nawaombeni ndugu zangu Watanzania mliopiga kura nyingi na za kishindo kwa mzee wetu Lowassa, kura zaidi ya milioni sita, mtusamehe kwa yeye kushindwa kuwashukuru. Serikali imeminya uhuru wa demokrasia kwa kuzuia mikutano ya hadhara,” alisema.

Alisema Lowassa anapenda
sana kuwafikia wananchi kupitia mikutano ya hadhara ili awashukuru kwa
heshima kubwa waliyompa, lakini ameshindwa kutokana na mikutano hiyo kuzuiwa.
Hata hivyo, alibainisha kuwa Lowassa hatachoka kuwasemea wananchi hao kero zao na ana imani kero hizo
Rais Magufuli na viongozi wa CCM wanazisikia na watazifanyia kazi.
Kada huyo wa Chadema na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, alisema wananchi wanapaswa kumuelewa Lowassa na Ukawa kwa jumla kuwa wanapenda kufanya mikutano ya hadhara ila wamezuiwa.
Alisema viongozi wanapenda kuwafikia wananchi ili kusikiliza changamoto zao za maisha, pia kuzungumza pamoja kuhusu mustakabali wa nchi, lakini hilo sasa ni gumu kufanyika.

“Sisi wachambuzi wa
kisiasa tunaona dhahiri kabisa ishara ya kifungo cha kisiasa kwa Lowassa na viongozi wa vyama vya upinzani nchini.
Haya yamefanywa makusudi na watawala ili kuminya
demokrasia,” alisema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: