JE, wajua kama maji ya tunda la tikitimaji ni msaada mkubwa kwa kinababa katika kuwasaidia kupata raha za ndoa pengine kuliko hata dawa maarufu kwa kazi hiyo kama zile za ’viagra’?


Hakika, inawezekana taarifa hizo ni mpya na pengine, ikawa ngumu kueleweka, lakini ukweli ndiyo huo, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa taarifa za majarida mbalimbali ya lishe na afya na pia maelezo ya baadhi ya madaktari waliowahi kuzungumza na gazeti la  Nipashe.

Kwa mujibu wa taarifa hizo za lishe na afya, ni kwamba maji ya tunda la tikitimaji huwasaidia zaidi wapendanao katika kuwapatia raha ya tendo la ndoa kutokana na wingi wa viinilishe vilivyomo kwayo.

Inaelezwa kuwa miongoni mwa viinilishe hivyo katika juisi ya tikiti ni pamoja na beta-carotene, folate, vitamin C, vitamin B5 na pia kiwango kidogo cha vitamin B1, B2, B3 na B6.

Aidha, inaelezwa kuwa mbali na maji ya juisi ya tikiti, tunda lenyewe pia ni tajiri wa viinilishe vingine muhimu vya mwili kama madini ya calcium, magnesium, phosphorus, potassium, sodium na pia kiwango kidogo cha shaba, chuma na zinki. Vimo pia viinilishe vyenye kumhakikishia mlaji vitamin A, anthocyanins na virutubisho vingine vingi.

“Wingi wa viinilishe hivi ndiyo chanzo cha maji ya tikiti na pia tikiti lenyewe kuwa na msaada mkubwa kwa walaji wake, hasa kinababa ambao huongezewa nguvu katika tendo la ndoa,” mmoja wa wataalamu aliiambia Nipashe.

Mbali na kuwasaidia wanaume katika kuwaongezea nguvu ya tendo la ndoa, faida nyingine za maji ya tikiti na tunda lenyewe pia ni kusaidia kuimarisha misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri. Pia faida nyingine kati ya nyingi ni kumuondoa mlaji katika hatari ya kupatwa na shinikizo la damu.

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanywa hivi karibuni na Dk. Pallangyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, asilimia 30 ya wanaume waliohusishwa katika utafiti jijini Dar es Salaam walikutwa na matatizo ya kuwa na upungufu wa nguvu za kiume.

Kwa sababu hiyo, inaelezwa kuwa ulaji mzuri wa matikiti maji unaweza kuwa mkombozi kwa walio wengi, kama ilivyo kwa watu wengine nje ya Dar na kwingineko duniani.

“Hata hivyo, muhimu kutambua hapa ni kwamba, faida hizo za matikiti kwa kinababa hupatikana kwa ulaji mzuri wa matunda hayo kungali mapema,” daktari mmoja bingwa wa wa masuala ya lishe aliiambia Nipashe jana na kuongeza:

“Isije kueleweka vibaya kuwa labda mtu akiwa na tatizo la nguvu za kiume ndiyo ale matikiti sasa ili akamridhishe mwenzake, hapana. Bali walaji wa matunda hayo ndiyo wenye kunufaika kwa kuimarisha afya zao na kuzuia uwezekano wa kupata matatizo ya aina hiyo.


“Watu ambao hawajaanza kusumbuliwa na nguvu za kiume ndio linaweza kuwasaidia lakini wale ambao wana matatizo hayo tayari haiwezi kuwa tiba tosha kwao,” alisema.

Akifafanua zaidi, mtaalamu mwingine alisema ulaji wa matikiti na pia matumizi ya juisi yake waweza kuchukuliwa kuwa bora zaidi kiafya kuliko hata matumizi ya dawa zinazotengenezwa viwandani, lakini hilo halimaanishi kwa wale wenye matatizo tayari au kutaka kushiriki tendo la ndoa na wenzi wao, bali wale wanaokula matunda hayo mara kwa mara na kuchukulia kuwa ni sehemu ya mlo wao.

“Misisitizo ni kwamba matikiti siyo dawa ya matatizo ya nguvu za kiume, bali ni kama kinga ya tatizo hilo kwa kina baba wanaotumia matunda hayo vyema.

Ni zaidi ya dawa za madukani kwa maana ya kumpa mtu afya njema, lakini siyo dawa kwa wenye matatizo,” alifafanua.

FAIDA ZAIDI

Inaelezwa kuwa kwenye tikiti maji kuna vitu vitatu muhimu kwa afya ya mapenzi ambavyo ni  ‘lycopene’, ‘Beta-carotene’ na ‘Citrulline’ ambavyo husaidiwa kuweka mishipa ya damu katika hali ya utulivu.

Aidha, tikitimaji inafafanuliwa zaidi kuwa ni ‘viagra ya asili’ inayoweza kutumika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa watu wa jinsia zote mbili bila kukuacha na madhara yoyote mabaya.

Kwenye tikitimaji hasa mbegu zake kuna kitu kingine kinaitwa ‘L-arginine’ ndicho ambacho huhusika na kuongeza nguvu za kiume.

Mbegu za tikitimaji zimeonyesha matokeo mazuri katika kuimarisha nguvu za kiume hata kwa wazee kabisa.

“Unachohitaji kwa mlaji ni kula tikitimaji kila siku ikibidi… tena na mbegu zake. Hapo utaimarisha afya yako kwa kiasi kikubwa,” anasema mmoja wa wataalamu wa lishe.

Pia lina Vitamini A ndani yake ambayo huboresha afya ya macho na Vitamini C ambayo huimarisha kinga ya mwili.

Pia tikitimaji husaidia kuponyesha jeraha, hukinga uharibifu wa seli, huboresha afya ya meno na fizi na Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema.

Tikitimaji pia hubadilisha protini kuwa nishati, chanzo cha madini ya potasiamu, husaidia kushusha na kuponya shinikizo la juu la damu na hurahisisha mtiririko wa damu mwilini.

Faida nyingine, huondoa sumu mwilini na ondoa sumu mwilini, huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake, husaidia wenye kisukari, husafisha figo na huzuia na  kutibu kansa mbalimbali.

Kadhalika husaidia wenye magonjwa ya moyo, huzuia na kutibu pumu, kufungua choo, hufanya ngozi ing’ae, huhamasisha kuota nywele, husaidia kupunguza uzito na kuimarisha mifupa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: