
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Kila mtu katika eneo la kazi napenda kusikilizwa, kuheshimiwa na hata kuona mawazo na mapendekezo yake yanafanyiwa kazi. Mara nyingi hiki kitu si rahisi hata kwa wale wenye nyadhifa za juu katika taasisi. Wapo wanaohisi wanadharauliwa na hata wanapotoa wamazo yao maranyingi hayasikilizwi.
Ifahamike kuwa, kuwa na mamlaka haikufanyi moja kwa moja kuwa na ushawishi. Mamlaka unayapata kutokana na wadhfa au cheo chako ulichopewa lakini ushawishi ni nguvu inayojengwa japo kwa baadhi ya watu wanaushawishi kwa asili.
Ushawishi husaidia katika kuaminiwa katika masuala mbali mbali na watu wenye ushawishi wana nafasi kubwa ya kupewa dhamana ya uongozi na mawazo yao kusikilizwa na kutekelezwa. Ushawishi huleta nguvu ambayo wakati mwingine mamlaka au cheo haviwezi kutoa; unaweza kuwa na mamlaka (authority) lakini ukakosa nguvu (power) ya kushawishi au kutoa maelekezo na ya kutekelezwa. Ushawishi siyo muhimu kwa viongozi pekee lakini kwa kila mtu katika eneo la kazi au biashara.
Kuwa mfanisi na mbobezi wa kazi yako
Inawezekana kabisa eneo unalofanyia kazi kuna wataalam watehema au fani yote yoyote ile zaidi ya mmoja lakini tatizo lolote linapotekea lihusio fani hiyo kuna mtu ambae ujuzi wake hautiliwi mashaka hata kidogo. Watu wa aina hii huwa na ushawishi mkubwa sana makazini kwani hata mawazo yao hupewa uzito mkubwa. Ufanisi kazini na ubobezi katika fani fulani hujengwa kwa kufanya kazi kwa bidi na utayari wa kujifunza vitu vipya kila leo. Ukitaka kuwa na ushawishi kazini kwako hakikisha unaielewa vizuri kazi yako na uko tayari kujifunza hata kwa wale walio chini yako katika muundo wa taasisi.
Jenga Uaminifu
Moja ya vitu vinavyotufanya tuonekane watu wa kawaida au pengine tuepukwe na wafanyakazi wenzetu katika mambo mengi ni kukosa uaminifu. Uaminifu haupimwi kwa kuangalia matumizi ya rasilimali mbalimbali ikiwemo mali za ofisi na hata muda. Hakikisha kile chochote unachopewa kukitumia kama nyenzo ya kukuwezesha kufanya kazi vizuri unakitumia kwa kuzingatia maadili ya kazi na kuepuka kutoa ahadi za uongo au zisizotekelezeka. Fahamu kuwa kurudisha uaminifu ni kazi sana pale mtu anapoupoteza kwa namna moja ama nyingine. Matendo kama rushwa, ubadhilifu, uongo na mengineyo ni ya kuepukwa ili usivunje uaminifu kwa wengine.
Tenda haki
Katika kila jambo unalotakiwa kulifanya hasa katika kutoa maamuzi hakikisha unatenda haki. Hii inaenda sawia na kutoa maoni juu ya mambo au watu wengine kwani watu kupenda kutathmini kama kweli wewe ni mtenda haki hata kupitia maoni unayotoa juu ya wengine. Ubaguzi na upendeleo hupunguza au huondoa kabisa ushawishi wa mtu kwa wengine. Hakikisha maamuzi yoyote unayoyafanya ni matokeo ya uchambuzi na fikra sahihi juu ya jambo husika. Maamuzi ya kukurupuka husababisha kutoa maamuzi yasio sahihi yanayoweza kusababisha kumnyima mtu haki yake pengine hata bila kukusidia.
Shirikiana na mwenzako
Watu humuunga mkono yule wanayedhani kuwa yupo pamoja nao. Kwa sababu mbalimbali wapo wanafanyakazi katika taasisi ambao huamua kujitenga na wenzao. Wapo wanaoamini kuwa na cheo ni sababu ya kuweka ukuta na wengine bila kujua kuwa cheo ni taraja linaloweza kutumika katika kujenga mahusiano mazuri na wengine. Hata kama unamajukumu mengi hakikisha unapata muda wa kujumuika na wenzako katika matukio mbali mbali hata chakula cha mchana na kufanya mazungumzo nao.
Epuka makundi yasiyo na tija
Kwa kuzingatia kuwa binadamu yoyote yule ana asili ya kujihusisha na kikundi au vikundi fulani kama sehemu ya maisha ya kila siku hili ni suala lisiloepukika. Pamoja na hayo katika taasisi nyingi watu hutengeneza makundi ambayo husababisha migogoro na mifalakano kazini. Makundi ambayo huonesha dhahiri kuwa yanachuki na mtu au kikundi fulani. Epuka kuwa mmoja ya watu wa aina hii kwani itakusababishia ukubalike na wale tu uliyonao kundi moja na kuchukiwa na wengine. Fanyika sababu ya kuunganisha makundi ya aina hii kwani ni moja ya sifa kuu ya kiongozi yoyote. Tambua kuwa makundi yanayojengwa kwa misingi ya chuki, majungu na uhasama uwa hayadumu kwa muda mrefu na pia hugawanyika na kutengeneza makundi mengine madogo madogo ndani ya makundi hayo.
Ishi katika misingi
Maisha yasiyoyumbishwa yumbishwa na watu au matukio ni yale yaliyojengwa katika misingi bora. Ni vyema kuhakikisha kuwa maisha unayoishi yanaendesha na misingi fulani na ifahamike kwa wengine. Hata kama taasisi nzima itaonekana inawafanyakazi wanaopenda kupokea au kutoa rushwa kuna watu ambao misingi ya maisha yao ipo kinyume kabisa na jambo hilo hii huwajengea sifa njema kazini na kuongeza ushawishi. Misingi kama haki, usawa, upendo, ushirikiano, na mingine mingi huwafanya watu waishio kupitia kwayo kuwa na ushawishi na kusifika maeneo ya kazi.
Kuwa msikivu
Moja ya njia ya kujifunza ni kukubali kuwa wewe si mkamilifu na kusikiliza maoni ya watu wengine kwa lengo la kujifunza. Ni vyema kuwa na msimamo katika tuyafanyayo lakini tuache nafasi ya kuwasikiliza wengine bila kujali nyadhfa na vyeo vyetu. Usikivu unaendana na umakini katika kusikiliza matatizo na shida za wengine na kuwa tayari kuwasaidia pale inapowezekana.
Kuwa makini na maisha yako nje ya ofisi.
Wapo wanao amini kuwa maisha mtu anayoyaishi nje ya ofisi hayana uhusiano au athari kwenye maisha yake ya kazini. Ukweli ni kuwa maisha yako hasa tabia na mwenendo wako nje ya ofisi yana nafasi kubwa sana katika kuujenga au kuubomoa ushawishi wako kazini. Tabia kama ulevi wa kupindukia, kukosa uaminifu, lugha zisizo za staha, uasherati na nyingine zisizofaa zinaweza kufanyika nje ya eneo lako la kazi lakini likakuharibia sifa njema hado eneo lako la kazi na kupunguza au kuondoa ushawishi. Ni vyema kuishi maisha ya staha katika eneo lolote lile ili kuongeza ushawishi na kukusaidia katika maeneo mengine hasa kazini kwako.
Post A Comment: