Mshambuliaji fundi wa klabu ya wenkundu wa Msimbazi Simba SC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ibrahim Ajibu, ameondoka klabuni hapo na kutimkia nchini Msri kwa ajili ya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. 


Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo awali zilidai kuwa Ajibu ameondoka bila kutoa taarifa kwa uongozi wa klabu, lakini baadaye meneja wa timu hiyo Musa Hassan Mgosi amethibisha kuwa uongozi una taarifa na umetoa baraka kwa mchezaji huyo kwenda kutafuta nje ya Tanzania.

"Ajibu kaenda Misri kwajili ya majaribio na kapata ruksa ya viongozi kama ilivyo ada ya klabu ya Simba,  Simba haimzuii mchezaji wake akipata timu ya nje" Amesema Mgosi.

Ingawa Mgosi amesita kutaja timu ambayo Ajibu anakwenda, lakini zinaeleza kuwa anakwenda katika timu ya Harass El Hadood.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: