Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana amesema endapo angepata fursa ya kuonana na Rais John Magufuli angemshauri aondoe ukuta uliopo baina yake na viongozi wengine wa kisiasa kwa kukaa meza moja ya mazungumzo hasa kwa mambo ya msingi ya nchi.


Kauli ya Profesa Bana imetolewa wakati vyama vya siasa vikimshutumu Rais Magufuli kwa kuvibana baada ya Serikali yake kupiga marufuku mikutano yote ya vyama na badala yake akisema siasa za majukwaani zifanyike 2020 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Profesa Bana ambaye alikuwa akijibu swali la mwandishi wetu kuhusu jambo ambalo angemshauri Rais endapo angepata wasaa wa kukutana naye alisema: “Atengeneze jukwaa litakalokuwa linamwezesha kukutana na viongozi wenzake wa kisiasa, aitishe hata mkutano ili wajadili mambo muhimu. Anaweza kuongea na viongozi wenye vyama vyenye wabunge au vyama vyote vya kisiasa, hili ni suala muhimu sana.”

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: