BEKI wa pembeni wa klabu ya Simba, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amefunguka juu ya hatma yake ndani ya kikosi hicho akisisitiza bado ni mali ya halali ya timu hiyo.


Akizungumza  jana, Tshabalala, alisema mkataba wake na klabu hiyo umebakia miezi sita, lakini anaipa heshima timu hiyo linapokuja suala la hatma yake.

Kauli ya mchezaji huyo inapingana na ile ya uongozi wa juu wa timu hiyo ambao walikaririwa wakisema nyota huyo bado ana mkataba wa mwaka mmoja. 

"Kwa sasa nimepumzika na nisingependa kuongea sana kuhusu hayo mambo, ila mimi bado mali ya Simba japo mkataba wangu umebakiza miezi sita kumalizika," alisema Tshabalala.

Aidha, alipoulizwa kama ameanza mazungumzo na klabu hiyo kwa ajili ya mkataba mpya, Tshabalala, alisema jambo hilo linashughulikiwa na meneja wake.

"Mambo yakiwa tayari mtafahamu tu, lakini kuhusu mkataba mpya au kitu kingine, meneja wangu anafuatilia, tuwe na subira," alisema beki huyo wa pembeni ambaye pia anachezea timu ya Taifa 'Taifa Stars'.

Tshabalala, alisema yeye ni mchezaji na siku zote mpira ndio maisha yake, hivyo ni makini kwa kila jambo linapokuja suala la usajili au kupata mkataba mpya.

Juzi katibu Mkuu wa Simba, Patrick Kahemele, alisema timu hiyo ipo kwenye mazungumzo na Tshabalala kwa ajili kumuongezea mkataba mpya.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: