MWENYEKITI wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema atampiga marufuku Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara kama hatamtambua kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.

Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa CUF kwenye mkutano wa ndani mkoani Geita.

Ziara ya Lipumba imefanyika wakati Maalim Seif akiwa amesambaza barua kwa viongozi wa CUF wa wilaya zote nchini akiwataka wasishirikiane na Profesa Lipumba huku akionya atakayekaidi atachukuliwa hatua.

“Kama Maalim Seif hatambui kuwa mimi ni mwenyekiti wake, huku mimi nikimtambua kuwa Katibu Mkuu wangu, basi naye tutamzuia kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara,” alisema Lipumba.

Profesa Lipumba alisema hana tatizo na wananchi wa Zanzibar wala kiongozi wa upinzani atakayetetea watu hao na kuongeza kuwa yeye amekuwa mstari wa mbele kutetea Wazanzibari.

“Mimi natambua kuwa ndiye mwenyekiti halali wa chama hiki na mwenye mamlaka ya kumwondoa mwenyekiti au katibu ni mkutano mkuu wa chama na lazima theluthi moja ya wajumbe watoke Bara na theluthi nyingine Zanzibar, lakini mkutano huo haukufanyika wala muhtasari haupo,” alisema Profesa Lipumba.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: