Simba imefanya usajili wa kishindo katika dakika za mwisho kwa kuwasajili wachezaji wawili wa kimataifa Asante Kwasi na Domingos Anthonio.
Simba imempa mkataba ya miaka miwili beki Mghana Kwasi akitokea Lipuli pamoja na Domingos akitokea Ferroviario de Beira ya Msumbiji
Mbali ya kuwasajili nyota hao katika usiku huo wa Desemba 15, vinara hao wa Ligi Kuu Bara wameacha wachezaji watatu kati ya hao wawili wa kigeni na mmoja mzawa.
Mshambuliaji Laudit Mavugo ametolewa kwa mkopo katika ligi kuu ya nchini Oman, pia Jamal Mnyate amejiunga Lipuli kwa mkopo wakati nahodha Mzimbabwe Method Mwanjali akiachwa kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Post A Comment: