
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MAHAKAMA ya mjini London imetoa ruhusa kwa mwili wa binti wa miaka 14
aliyefariki kwa ugonjwa wa saratani kuhifadhiwa katika vimiminika
maalumu kama alivyotaka ili kuja kuamshwa baadaye dawa za saratani
anayougua itakapopatikana.
Binti huyo ambaye jina lake limehifadhiwa aliomba mahakama kumpa haki
ya kuhifadhiwa kwa kuwa hataki kufa akiwa mtoto ingawa anajua ugonjwa
anaougua utamuua.
Ruhusa hiyo ya kutekelezwa kwa matakwa yake imetolewa huku baba yake
mzazi akiwa anapinga mtoto wake kuhifadhiwa kwa kauli kwamba hata kama
ataamshwa miaka 100 ijayo au 200 atakuwa hana mtu anayemtambua ambaye ni
ndugu yake.
Binti huyo ambaye aliomba nafasi ya kuhifadhiwa katika mfumo huo
maalumu akisubiri kuamshwa baada ya dawa kupatikana, ombi lake lilikuwa
linaungwa mkono na mama yake mzazi.
Jaji wa mahakama kuu alisema kwamba ombi la binti huyo ni vyema
kusikilizwa na kwamba mama mzazi aruhusiwe kuona namna bora ya
kumhifadhi binti yake. Binti huyo ambaye alikufa Oktoba mwaka huu, mwili
wake tayari umeshapelekwa Marekani kwa kuhifadhiwa.
Taarifa ya shauri hilo la aina yake, ndio kwanza imetolewa na
mahakama. Binti huyo ambaye hakutajwa jina lake na ambaye alikuwa
anaishi mjini London, Uingereza katika siku za mwisho za uhai alikuwa
anajifunza kwa bidii masuala yanayohusu hifadhi kusubiri kuamshwa baada
ya dawa za ugonjwa kupatikana.
Mfumo huo ambao kiingereza unajulikana kama Cryonics (neno
lililotolewa kutoka lugha ya Kigiriki) huwezesha kuhifadhiwa kwa mwili
wa marehemu katika kiwango cha chini cha joto na mara nyingi ni chini ya
hasi 130 sentigredi, kusubiri maendeleo ya sayansi katika ugunduzi wa
dawa kwamba mwili huo utatibiwa na kuamshwa kuendelea na maisha
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: