Ofisa Mtendaji Mkuu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Acacia, wametangaza kujiuzulu kuanzia jana Novemba 2, 2017.


Kupitia barua yake, Ofisa Mtendaji Mkuu, Brad Gordon amesema anataka kurudi nyumbani kwao Australia kusimamia masuala ya familia yake wakati kwa upande Ofisa Mkuu wa Fedha, Andrew Wray akisema amepata fursa nzuri zaidi.

Pamoja na hatua hiyo.. taarifa hiyo imesema kuwa bado wataendela kuwa chini ya kampuni hiyo mpaka mwisho wa mwaka huu.

Tayari Bodi ya Acacia imewataja Peter Geleta ambaye atakuwa Mkurugenzi Mkuu na Jaco Maritz atakachukua nafasi ya Andrew Wray aliyekuwa Mkurugenzi wa fedha.

Wote wawili walioteuliwa walikuwa watendaji wa Acacia kwa muda mrefu ambapo Geleta alikuwa mkuu wa oganaizesheni wakati Maritz alikuwa meneja mkuu wa idara ya fedha.

Kwa miezi miwili iliyobaki, makabidhiano ya ofisi yataendelea kufanyika mpaka Januari Mosi, mwakani yatakapohitimishwa na uongozi mpya kuendelea kutekeleza majukumu yake.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: