Rais John Magufuli ametoa miezi miwili kwa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kupeleka umeme wa megawati 10 katika kiwanda cha vinywaji baridi cha kampuni ya Bakhresa Products Group kilichopo Mkuranga, Pwani.


Rais amesikitishwa na kitendo cha shirika hilo kutochangamkia fursa hasa katika viwanda ambavyo ndio wateja wao wakubwa.

"Nashindwa kuelewa hvi hawa Tanesco watawezaje kufanya biashara kama hawataki kuwafikia wateja wao. Nataka kufikia Disemba mwaka huu umeme uwe umefika hapa," amesema.

Amelitaka shirika hilo kutambua kipaumbele cha Taifa ambacho ni kuwa ni uchumi wa viwanda. Amesema viwanda vinahitaji umeme wa kutosha kwasababu vinasaidia kuzalisha ajira.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: