Leonardo Ulloa alifunga mabao mawili kuisaidia Leicester City kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Swansea City, na kuzidi kuiweka klabu hiyo kukaribia ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.


Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa King Power jioni ya leo, unaifanya Leicester kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 8 dhidi ya wanaowakimbiza kwa ukaribu klabu ya Tottenham.

Mbali ya kumkosa mshambuliaji Jamie Vardy aliye na adhabu, bado vijana wa kocha Claudio Ranier waliweza kupata mabao hayo kupitia kwa Riyad Mahrez, Jose Leonardo Ulloa aliyefunga mara mbili na Marc Albrighton.

Nayo Arsenal ilibanwa mbavu, baada ya kwenda sare ya 0-0 na Sunderland ugenini kwenye uwanja wa Stadium of Light.

Matokeo hayo yanawabakisha washika mitutu hao, nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza, wakiwa na vita na Manchester City kugombea kumaliza nafasi ya 3.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: