ads

Baada ya  Hitmaker wa My Life Dogo Janja kufunguka kuchukizwa na msimamo wa rapa Young Dee kuhusu video aliyoipost meneja wake Babu Tale akiwa na msanii mkongwe Chid Beenz, Young Dee amesema hajalishwi na maneno ya Dogo Janja.

Kupitia kipindi cha Planet Bongo East Africa Radio Young Dee amesema ameshazoea maneno hasi (Negative) kutoka kwa watu hivyo siku hizi hayamshtui na wala hajali chochote kuhusu maneno hayo.

Kuhusu tuhuma za kutumia madawa ya kulevya Young Dee ameendelea na msimamo wake ule ule kuwa hatumii madawa bali ni fununu tu zinazozushwa juu yake.
Hata hivyo alivyoulizwa kuhusu post ya Dogo Janja ya kumdiss alisema hajaiona,hafatilii na hayo ni mambo negative ambayo huwa hapendelei kuyapa kipaumbele.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: