Jukwaa la wahariri nchini Tanzania TEF limeelezea kutoridhishwa kwake na
uamuzi wa uongozi wa Bunge wa kuzuia bunge kutoonesha moja moja na
hivyo kutaka uamuzi huo kufikiriwa upya.
Jukwaa hilo limesema kuwa uamuzi huo umekuwa ukiathiri wananchi
pamoja na wanahabari wanaoripoti habari za bunge mjini Dodoma kushiriki
na kupata taarifa.
Mwenyekiti wa TEF Theophil Makunga na Makamu Mwenyekiti Deodatus
Balile wamesema ni wazi kwamba ushiriki wa wananchi katika kufuatilia
mwenendo wa bunge na wabunge wao umekwazwa sana na hatua hizi mpya.
Makunga amesema jukwaa hilo limejiridhisha kuwepo kwa mapungufu
makubwa matatu yanayosababishwa na mfumo huo unaotumiwa hivi sasa na
bunge.
Mapungufu hayo ni pamoja na habari zinazotoka ndani ya bunge kuchujwa
kupita kiasi, ubora wa picha zinazotolewa na ofisi ya bunge kwa
waandishi wa habari kuwa wa kiwango cha chini.
Mapungufu mengine ya mfumo huu kwa mujibu wa Makunga ni kukwaza haki
na uhuru wa wanahabari kufanya kazi yao kwa Uhuru lakini pia inawanyima
wananchi haki ya kupata kwa uhakika na bila kuchujwa kile kinachofanywa
na wawakilishi wao.
Kutokana na mapungufu hayo Makungu amesema kuwa jukwaa hilo limeanza
kuingiwa na hofu kuwa sababu zilizotolewa awali za kuzuia utangazaji wa
moja kwa moja wa Bunge kupitia TBC kuwa ni gharama, huenda hazikuwa za
dhati.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: