MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) leo anawasilisha
bungeni ripoti ya mwisho ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka
2014/15. Ingawa haijajulikana rasmi nini kilichomo ndani yake, baadhi ya
watu waliohojiwa wanatarajia CAG kubaini mchwa wanaotafuna fedha za
umma na namna ya kukabiliana nao.
Aidha wengine wanatarajia taarifa ya hali bora zaidi ya usimamizi wa
fedha za umma kuliko kipindi cha nyuma. Ripoti hiyo awali ilikuwa
imepangwa kuwasilishwa bungeni mwishoni mwa wiki (Aprili 22) kabla ya
kuahirishwa hadi leo.
“Ni kweli CAG atawasilisha ripoti kesho (leo) bungeni, ”Naibu Katibu
wa Bunge na Utawala, Joel Joel aliithibitisha juu ya
kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo. Miongoni mwa wabunge waliozungumza na
mwandishi wa habari hizi, wamesema wanatarajia CAG kuonesha mambo mazuri
kwa maana ya taasisi zilizofanya vizuri katika usimamizi wa fedha za
umma lakini pia mambo mabaya.
“Lazima ripoti itaibua madudu maana walizoea (watendaji serikali)
kana kwamba hapakuwapo na serikali,” alisema Mbunge wa Nkasi Kaskazini,
Ally Keissy na kusisitiza kuwa pamoja na wabunge wenzake, watamsaidia
Rais John Magufuli kupambana na ubadhirifu serikalini.
Keisy alisema akiwa mbunge, anaamini pamoja na wenzake, wanachosubiri
ni kuona ripoti hiyo na kuhakikisha wanaohusika na kuchezea fedha za
serikali, kabla ya kufikishwa mahakamani, wanarudisha fedha hizo.
“Atakachosema CAG sisi tutakuwa tayari kusimama kusaidia Rais aendelee
kupambana na ubadhirifu,” alisema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: