MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, hivi sasa yupo Uganda na atakaporejea tu kuungana na wenzake, basi atatua na familia yake.


Okwi aliondoka nchini wiki iliyopita baada ya wachezaji wa timu hiyo kupewa mapumziko mafupi ambapo wakati anaondoka alikuwa akisumbuliwa kifundo cha mguu.

Okwi alisema yupo kwao Uganda lakini bado anaendelea na matibabu ya kifundo cha mguu ambapo atakapopona, atarejea nchini akiwa na familia yake.

“Nipo huku naendelea na matibabu yangu ya kifundo cha mguu baada ya kuumia hivi karibuni na kunifanya nikose baadhi ya michezo ya ligi kuu.

“Niliondoka huko baada ya wachezaji wote kupewa mapumziko, lakini nimepanga nikirejea basi nitakuja na familia yangu ambayo awali niliiacha huku Uganda kwa sababu hivi sasa nataka niwe nayo karibu,” alisema Okwi ambaye ana mke na watoto wawili.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: