
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Pamoja na kuendelea na mazoezi jana, kikosi cha Simba kimewakosa wachezaji wake watatu wa kimataifa, wawili kutoka Uganda na mmoja kutoka Rwanda.
Haruna Niyonzima yuko kwao Rwanda akiwa amepewa ruhusa ya kwenda kuhani msiba pamoja na masuala kadhaa ya kifamilia.
Niyonzima alipewa ruhusa ya kuondoka baada ya mechi dhidi ya Lipuli ambayo mwisho iliisha kwa sare ya mabao 1-1.
Lakini Emmanuel Okwi ameendelea kubaki kwao Uganda kwa kuwa ni majeruhi na mkewe alijaaliwa kujifungua mtoto wa pili.
Pamoja na Okwi, Simba inamkosa Juuko Murshid ambaye yuko katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda, The Cranes kinachoshiriki michuano ya Chalenji.
Simba imefanya mazoezi chini ya kocha wake msaidizi, Masoud Djuma raia wa Rwanda kwa kuwa kocha wake mkuu, Joseph Omog pia alipewa mapumziko mafupi kwenda kwao Cameroon.
Post A Comment: