IMEELEZWA kuwa kasi ya ongezeko la watu nchini inatokana na jamii kutokuwa na elimu ya  afya ya uzazi inayochangiwa na umaskini ambapo mwanamke aliyefikia umri wa kuzaa anazaa watoto zaidi ya nane.


Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile

β€œTakwimu za utafiti wa hali ya afya na idadi ya watu mwaka 2015/2016 inaonyesha kasi ya ongezeko la idadi ya watu ni 2.7 na hali ya uzazi ni wastani wa watoto watano kwa kila mwanamke aliye kwenye umriwa kuzaa,’’ alisema Ndugulile.

Alisema wastani wa idadi ya watoto kwa mwanamke asiye na elimu ni watoto saba, wakati kwa mwanamke aliyefikia elimu ya sekondari ni watoto wanne na wale walio na hali ya umaskini mama anazaa watoto nane ikilinganishwa na yule mwenye uchumi mzuri anayezaa watoto watatu.

Alisema serikali ya awamu ya tano inahakikisha mtoto anayetakiwa kwenda shule kwa ngazi ya msingi na sekondari inagharamia elimu yao .

Aliongeza serikali inasisitiza ujenzi wa viwanda ili vijana wanaomaliza masomo ngazi mbalimbali wapate  ajira.Mwakilishi mkazi wa UNFPA  nchini, Jacqueline Mahon, alisema kumekuwapo na ongezeko kubwa la kutokuwa na usawa duniani la kipato, rasilimali na haki.

Alisema katika nchi nyingi zilizoendelea ikiwamo Tanzania, wanawake wengi wanakosa nguvu katika kufanya maamuzi juu ya masuala ya afya ya uzazi, ikiwamo juu ya maamuzi ya muda na wakati gani wa kushikaujauzito.

β€œUsawa na ustawi wa watu wote ni msingi wa malengo ya maendeleo endelevu ya dunia ili kuyafikia, tunahitaji kuwajengea uwezo wale ambaowanaonekana wako nyuma hasa wanawake na watoto wa kike,” alisema.

Cristina Kwayu, kutoka UNFPA, alisema  kila mwaka idadi ya watu inaongezeka ambapo kwa sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na watu zaidi ya milioni 50.

Aliongeza kuwa changamoto ya kasi ya idadi ya watu imechangia watoto kutopelekwa shule, mtoto kuzaa mtoto hata madarasa kutojitosheleza kutokana na kila mwaka watoto kuongezeka. 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: