KLABU ya soka ya Mtibwa Sugar haina mpango na usajili wa dirisha dogo linaloendelea kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na kocha wao, Zuberi Katwila, kuweka wazi kuwa hahitaji kuongeza wachezaji wapya.


Akizungumza na  gazeti la BINGWA, Katwila alisema ana kikosi kipana ambacho kimeimarika kila idara ndio maana  hafikirii kufanya usajili katika dirisha dogo.

Alieleza kuwa anaweza kusajili iwapo  baadhi ya wachezaji waliopo sasa wataondoka na kuacha pengo katika  kikosi hicho.

β€œSina matarajio ya kusajili kwa sababu  nawaamini wachezaji waliopo kwani  wengi ni vijana na baadhi yao bado hawajapata nafasi ya kucheza,” alisema Katwila.

Wachezaji waliosajiliwa katika dirisha kubwa lililofungwa Agosti 6, mwaka huu ni Hassan Isihaka kutoka African Lyon, Hassan Dilunga (JKT Ruvu) na Kelvin Sabato (Majimaji).

Kikosi cha Mtibwa kinashika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu, baada ya kufikisha pointi 18  huku Simba wakiwa kileleni kwa idadi ya mabao mengi, lakini wakiwa na pointi 23 sawa na Azam.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: