Kamanda wa Polisi nchini, Simon Sirro amewataka wazazi ambao watoto wao hawakuhamishwa shule na hawajui mahali walipo kuripoti polisi.


Hatua hiyo inatokana na kusambaa kwa taarifa ya kupotea kwa watoto 1,300 wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani kupotea kusikojulikana.

β€œNi taarifa ya muda mrefu, kipindi cha mwaka jana na mwaka huu, ni zaidi ya mwaka mmoja niliipata Wizara ya Elim kule ndiyo maana nimeelekeza wazazi ambao hawawaoni watoto wao kutoa taarifa.

β€œMaana kama mtoto humuoni shuleni wala nyumbani si lazima uripoti,” amesema Kamanda Sirro.

Kupotea kwa watoto hao kumezua sintofahamu kutokana na wazazi wa watoto hao kutiripoti tukio hilo polisi.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: