ads

Mshambuliaji mkongwe wa Majimaji, Danny Mrwanda amejiunga kwa mkopo na timu ya JKT Mlale.


Mrwanda aliyewahi kutamba akiwa Simba na Yanga na katika klabu mbalimbali za barani Asia alipokuwa akicheza soka la kulipwa amejiunga na JKT Mlale inayoshiriki ligi daraja la kwanza kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Klabu hiyo kupitia kwa Ofisa Habari wake, Onesmo Ndunguru ilisema mshambuliaji huyo ameridhia kutua katika timu hiyo bila kinyongo chochote.

Ndunguru alisema kuwa kutokana na changamoto za kukosa namba uwanjani wameona ni bora akaitumikie JKT Mlale kuliko kukaa benchi na kupungua kiwango chake.

“Bado tuna mkataba nae  wa mwaka mmoja  ambao huo mkataba atakwenda kuumalizia huko Mlale ambako uongozi umempeleka kwa ajili ya kumfanya aendelee kuonyesha uwezo wake na timu hiyo ya daraja la kwanza,’’alisema Ndunguru

Mrwanda alisema kutua kwake JKT Mlale siyo kwamba ameshuka kiwango bali ni timu kama zilivyo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema ‘Ninaimani ninakwenda kuonyesha kipaji kama nilivyofanya kwa timu zingine za Bara ninaiona ni timu nzuri na kwa ushirikiano pamoja na kujituma tutaivusha JKT Mlale kwenda Ligi Kuu.”

Kuhusu usajili wa wachezaji wapya katika kipindi hiki cha dirisha dogo linalotarajia kufungwa Disemba 15 mwaka huu,Ndunguru alisema uongozi hadi sasa haujaweka wazi  ni wachezaji wangapi watasajili na nafasi zao.

“Kufanya usajili siyo lazima kwani kikosi ni kikubwa, kocha Habib kondo akiwanoa vyema wanaweza kuisaidia timu kumaliza ligi katika nafasi nzuri zaidi kuliko kujaza wachezaji halafu matunda yasionekanae.”
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: