STRAIKA wa Yanga, Donaldo Ngoma alitarajiwa kutua nchini jana akitokea kwao Zimbabwe, lakini uongozi wa klabu yake umepanga kumchukulia hatua kali kama atatoa majibu yasiyoridhisha.


Ngoma alipewa ruhusa ya kwenda Zimbabwe kwa mapumziko madogo kutokana na kuwa majeruhi, lakini alikaa huko zaidi ya muda aliopewa bila kutoa taarifa.

Kutokana na hilo, mabosi wake wamepanga atakapofika tu aeleze kilichomfanya achelewe na kama atatoa majibu yasiyoridhisha, atachukuliwa hatua kali.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema: "Taarifa ya kurudi kwake ilikuwa jana na atakapofika, atatakiwa aeleze kilichomchelewesha na kama hatakuwa na sababu zisizo na mashiko, itabidi ahadhibiwe. Amepewa muda wa kujieleza kwa sababu yeye ni binadam,  huenda alikuwa na sababu zenye mashiko.”

Ngoma alipata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo wao na Mtibwa Sugar jijini Dar es Salaam, maumivu

hayoyaliyomweka nje ya uwanja akakosa mechi nne za ligi ikiwemo ya watani wao Simba.

Hata hivyo, inadaiwa mchezaji huyo yuko mbioni kujiunga na Singida United inayofundishwa na kocha wake wa zamani, Mholanzi Hans Pluijm.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: