ads

MSANII wa Bongo Fleva, Vanesa Mdee ‘V Money’, amesema kuwa bado hajafikia hata robo ya malengo aliyojiwekea kuyafanya kupitia fani ya muziki.


Akizungumza na gazeti la Mtanzania V money alisema anakabiliwa na kibarua kizito kuhakikisha anasonga mbele na kupiga hatua zaidi ya sasa.

Alisema wasanii wengi wamekuwa wakimpa pongezi na kumsifia kwa hatua aliyofikia, anashukuru  ila bado upande wake hakuna chochote anachoweza kujisifia.

“Mimi kama mimi bado naona sijafikia hata robo ya malengo ninayotarajia kuyapata kupitia muziki, ila nashukuru wale wanaonipongeza kila kukicha,” alisema V Money.

Mwanadada huyo anayetamba na wimbo wake wa Kisela, alieleza kuwa ataendelea kupambana zaidi na zaidi ili kuutangaza muziki wa Tanzania na kutangaza kipaji chake.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: