Kazi imeanza. Mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam ndiyo inapigiwa hesabu ya viwanja vyake kutumika kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika ya Vijana (AFCON).


Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya 2019 na tayari Serikali imekubali uenyeji huo na jana Jumamosi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alizindua kamati ya kitaifa ya mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini, Yusufu Singo alisema; "Tunategemea kuwapokea wataalamu kutoka CAF wakati wowote kuanzia sasa maana tumeambiwa watawasili nchini haraka iwezekananvyo, huenda ikawa mwezi huu wa Novemba, pamoja na mambo mengine lakini kikubwa wanachokuja kukifanya ni ukaguzi wa viwanja vitakavyotumika.

"Tunategemea kuwapeleka katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dodoma na Dar es Salaam kisha wao sasa ndiyo watashauri ni viwanja vipi  ambavyo wanaona vinastahili kutumika kwenye AFCON na  vitu gani vya kuboreshwa zaidi," alisema Singo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: