MSHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi, amewahakikishia mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuwa baada ya kurejea kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara, hawatashuka tena hadi watakapotangazwa mabingwa wa kipute hicho.


Akizungumza na gazeti la  Bingwa juzi baada ya mchezo wao wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Okwi alisema wanajisikia furaha kurudi tena kileleni mwa ligi baada ya kupambana vilivyo dhidi ya wenyeji wao hao na kupata ushindi wa bao 1-0, shukrani kwa bao la dakika ya saba la Shiza Kichuya.

β€œLengo lilikuwa kupata matokeo ugenini, haijalishi tumechezaje, tumefanikiwa kupata pointi tatu ndio muhimu kwetu,” alisema Okwi.

Aliongeza kuwa kurejea kwao kileleni mwa ligi ni kama wameanza mbio zao za kuchukua ubingwa msimu huu, kwani hakuna timu itakayowashusha tena.

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Simba, Masudi Djuma, alikiri kuwa Mbeya City ni kiboko licha ya timu yake kuibuka na ushindi huo.

β€œ(Mbeya City) ni timu nzuri, inacheza vizuri ndio maana walitupa taabu kidogo kipindi cha pili. Ni jambo la kufurahisha kurudi tena kileleni, lengo letu ni kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Djuma alisema kikosi cha Simba kitabaki jijini hapa kuweka kambi wakisubiri mchezo wao na Prisons utakaopigwa Novemba 18, mwaka huu, ambapo watacheza mchezo mitatu ya kirafiki.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: