Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari, amekata rufaa kupinga hatua ya kuenguliwa wagombea wake wawili waliopitishwa kugombea udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa marudio unaofanyika katika kata tano katika Jimbo la Arumeru Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari, Nassari amesema kuwa amesikitishwa na uamuzi uliofanywa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo kwani hawakuzingatia kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi.
Nasari amesema amekata rufaa Tume ya Uchaguzi kupitia Mkurugenzi wa Taifa wa Uchaguzi kufikisha malalamiko yao kwani kutenguliwa kwa wagombea wao kutokana na kutofuatwa taratibu ikiwemo msimamizi wa uchaguzi msaidi kuwatengua wagombea wakati hana sifa ya kufanya hivyo.



Post A Comment: