NYOTA wawili wa kutumainiwa wa klabu ya Simba, Mlinda mlango Aishi Manula pamoja na kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya, wamepokea viatu vyenye thamani ya Sh 500, 000 kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo.


Wawili hao walikabidhiwa viatu hivyo aina ya CR7 Mercurial kutoka kampuni ya Nike, mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli, ulioisha kwa sare ya bao 1-1 uliopigwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa viatu hivyo, Manula alisema anajisikia fahari kupata zawadi hiyo kutoka kwa mashabiki hao ambao wameonyesha upendo wao kwake na kuahidi kuendelea kufanya vizuri ili kuwafurahisha zaidi.

β€œNi jambo zuri ambalo linatia hamasa ya kuendelea kujituma zaidi na kuisaidia timu kufanya vizuri zaidi katika michezo ya ligi kuu ili tuweze kutimiza malengo yetu,” alisema.

Naye Kichuya alisema zawadi hiyo itakuwa chachu kwake kufanya vizuri zaidi kutokana na upendo anaoonyeshwa na mashabiki hao, ambao wamekuwa wakiwaunga mkono katika harakati zao za kulisaka taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: