STRAIKA wa Mwadui FC Hassan Kabunda, muda wowote atasaini mkataba wa kuichezea Simba na kinachosubiriwa ni klabu hizo mbili zimalizane, akaanze maisha mapya.


Simba itamsajili mchezaji huyo mara tu mazungumzo  yatakapokamilika na Mwadui kumruhusu, kwa sababu bado ni mchezaji wao na wana mkataba naye.

"Siwezi kukataa ofa ya timu yoyote kama naona inalipa, mpira ndio kazi yangu kwahiyo kama Simba wananihitaji waje tuzungumze," alisema Kabunda anayeichezea Mwadui kwa msimu wa tatu sasa.

Hata hivyo, mchezaji huyo alisema, ili awe na amani Simba anataka kucheza kwa malengo na kuwa tegemeo kikosi cha Kwanza na pia, imboreshee maslahi, yawe mazuri zaidi ya anayoyapata Mwadui.

"Kwa sasa mpira ni kazi, kwahiyo hata dau kubwa ni kishawishi cha mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine ila kwangu nahitaji sehemu nitakayokwenda niwe na uhakika wa namba," alisema Kabunda.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: