
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Kiongozi mkuu wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa), Raila Odinga ameubadili muungano huo wa kisiasa kuwa “muungano wa kiharakati” ambao hautakuwa unawatambua wala kuheshimu viongozi wa Serikali ya Jubilee.
Odinga amesema hayo jana Jumatano Oktoba 25,2017 alipowahutubia wafuasi wake kwenye viwanja vya Uhuru Park, Nairobi siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi wa marudio kwa Urais.
"Hatutaitambua Serikali ambayo haitakuwa imechaguliwa kwa kuzingatia Katiba,” amesema akimaanisha utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.
"Hatutawaheshimu Uhuru, (Makamu wa Rais William) Ruto, wakuu wa mikoa, makamishna wa kaunti na wengine wote..." amesema Odinga.
Pia, amewataka Nasa kufanya maombi mbali na vituo vya kupigia kura au wabaki majumbani kwao leo Alhamisi Oktoba 26,2017 Kenya itakapofanya uchaguzi aliouita wa kinafiki.
"Msishiriki uchaguzi huo wa maigizo," amesema Odinga. Amewaeleza wanachama kwamba, "Nendeni mshawishi kila mmoja asishiriki uchaguzi huo."
Tofauti na tamko la awali, amewataka wafuasi wake wasithubutu kuingia mitaani akionya kuwa Serikali imesambaza polisi kwa ajili ya “kuwaua”.
Odinga ametoa tamko hilo baada ya Mahakama Kuu ya Kenya kuondoa kwa kiasi fulani giza lililozingira uchaguzi wa marudio kwa kura ya urais uliopangwa kufanyika kesho baada ya kutupilia mbali maombi ya kutaka uahirishwe ikisema haina mamlaka hayo kisheria.
Baada ya juhudi zote za kuzuia uchaguzi kukwama, Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati amelitangazia Taifa kwamba uchaguzi huo utaendelea kesho kama ulivyopangwa.
Amesema kazi ya usambazaji makaratasi ya kupigia kura na vifaa vingine ilikuwa inaendelea vizuri.
Chebukati amesema vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kesho Alhamisi Oktoba 26,2017 saa 12:00 asubuhi na kutakuwa na usalama wa kutosha.
"Hakikisho ambalo tume imepewa na mamlaka husika na vyombo vya usalama hasa kwa kuzingatia maendeleo yaliyofikiwa hadi sasa na tume, uchaguzi utaendelea kesho kama ulivyopangwa," amesema Chebukati alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za IEBC zilizoko jengo la Bomas.
Jengo hilo ndilo lililotangazwa katika Gazeti la Serikali kwamba kitakuwa kituo cha kujumlishia matokeo.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Chebukati aliongozana na makamishna wote watano kuthibitisha kwamba hakukuwa na mgogoro wowote ndani ya IEBC.
Post A Comment: