Rais  John Magufuli amefichua kuwa anapokea mshahara wa kila mwezi wa shilingi milioni 9 za Tanzania.


Hii ni robo ya mshahara ambao mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa akipokea iwapo takwimu zilizonakiliwa na Afrika Review miaka mitatu iliopita ni za kweli.

Rais Magufuli alifichua hayo katika taarifa ya moja kwa moja katika runinga mapema leo Jumanne katika hotuba kwa muungano wa serikali za mitaani wakati ambapo alikuwa akikisisitiza kuhusu umuhimu kwa kukabiliana na rushwa.

''Baadhi ya wanachama wa bodi za mashirika ya uma walikuwa wakisafiri hadi Dubai kufanya mikutano yao huko ili wajilipe marupuru mengi.Hivi sasa hawataki kile serikali yangu inachofanya''.

Credit - BBC
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: