WANASAYANSI nchini Ujerumani wanasema wamegundua kwamba kuna chembechembe hai kwenye pua ya mwanadamu ambayo inaweza kutumia kuua viini hatari.


Dawa nyingi za kuua viini vinavyosababisha maradhi hutolewa kutoka kwenye mchanga.

Lakini kutokana na hali kwamba viini vinavyosababisha magonjwa mengi vimeanza kuwa sugu na kutosikia dawa, wanasayansi wamekuwa wakitafuta njia nyingine za kupata dawa mpya.

Ripoti ya vipimo imebaini katika jarida la asili kwamba dawa aina ya Lugdunin, inaweza kutibu maambukizi ya maradhi yasiyosikia dawa.

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Tubingen nchini Ujerumani, waliogundua chembe hizo wanasema kuwa mwili wa binadamu ni chanzo cha dawa mpya ambazo bado hazijatumiwa.

Dawa ya mwisho kugunduliwa katika mwili wa binadamu ilipatikana mwaka 1980.

BBC
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: