JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kwa muda wa siku tano kupitia tozo za makosa barabarani, kimekusanya kiasi cha Sh. milioni 454.8


Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mambosasa alisema faini hizo zinatokana na operesheni ya ukamataji wa makosa mbalimbali ya barabarani kuanzia Alhamisi iliyopita hadi juzi.

Fedha hizo ukizigawa kwa siku maana yake ni kwamba jeshi hilo, lilikuwa likikusanya Sh. milioni 90.

Mambosasa alitaja idadi ya magari yaliyokamatwa kuwa ni 14,773, pikipiki 387, daladala 4,904, na magari mengine (binafsi na malori) ni 9,869.

Alisema idadi ya bodaboda waliofikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa helmeti na kupakia mishikaki ni 26.

β€œJumla ya makosa yaliyokamatwa ni 15,160 na fedha za tozo zilizopatikana ni Sh. milioni 454.8,” alisema.

Pia alisema magari yaliyokamatwa kutokana na kuchelewa kulipa faini kwa wakati zaidi ya siku saba ni 1,846 ambapo kiasi kilicholipwa ni Sh. milioni 178.5.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: