Serikali ya China imeisadia Serikali ya Tanzania fedha zaidi ya bilioni sita kwa ajili ya ukarabati na maboresho ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto M. James amethibitisha hilo na kusema hii ni mara ya sita uwanja huo kufanyiwa ukarabati na wafadhili hao ambao ulijengwa miaka kumi iliyopita. 

"Karibia bilioni sita zitakwenda kwenye eneo hilo sasa unaweza kuona kiasi gani cha fedha China wanatusaidia na huu ni msaada wala siyo mkopo wa kufanyia marekebisho na wanaleta watu wao kwa ajili ya maboresho na kuongezea teknolojia za kisasa zaidi kwenye uwanja huo, kwa hiyo sisi kwetu tunasema msaada huo ni muhimu sana kwa sababu ukijenga uwanja kuanzia hapo kila mwaka utahitaji kuboresha na kuweka vitu mbalimbali kuzidi kuimarisha" alisema Doto James 

Maeneo ambayo yatafanyiwa marekebisho katika uwanja huo ni pamoja miuondombinu yote ya uwanja, viti vya kukalia watazamaji, vyoo, kupakwa rangi na mfumo wa maji taka na maji safi, taa pamoja na mfumo wa usalama ndani ya uwanja huo. 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: