Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema leo Jumapili ataweka hadharani ushahidi wa tuhuma walizonazo kuhusu madiwani wa chama hicho waliojiuzulu wakisema ni kutokana na kuunga mkono utendaji wa Rais John Magufuli.


Lema na mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari wamewatuhumu madiwani hao wakisema uamuzi wao unatokana na rushwa.

Hata hivyo, madiwani hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikanusha tuhuma hizo.

Lema akizungumza na gazeti la  Mwananchi jana Jumamosi, amesema wataweka hadharani ushahidi huo kesho kabla ya Jumatatu kuupeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: