MHASIBU wa Shule ya Sekondari ya St. Joseph Cathedral ya jijini Dar es Salaam, Elizabeth Asenga, amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano au kwenda jela miezi 12, baada ya kukutwa na hatia ya kumwita Rais John Magufuli kilaza kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.


Mshtakiwa alilipa faini hiyo na kuachiwa huru.

Hukumu hiyo ilisomwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kusema mahakama yake imemwona mshtakiwa ana hatia.

Alisema upande wa Jamhuri uliita mashahidi saba kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.

"Mahakama hii inakutia hatiani dhidi ya mashtaka yanayokukabili," alisema Hakimu Shaidi kumuamuru Asenga "utalipa faini ya Sh. milion tano na ukishindwa kulipa faini, ukatumikie kifungo cha miezi 12 jela."

Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ili apunguziwe adhabu.

Mshtakiwa alidai kuwa mama yake mzazi ni mzee anayemtegemea, na ana watoto na familia nzima inayomtegemea yeye pia.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Agosti 6, 2016, akiwa anajua, aliwasilisha maneno kinyume cha sheria kupitia mtandao wa WhatsApp katika 'group' la wafanyakazi la STJ kwa nia ya kumtusi rais.

Mshtakiwa alinukuliwa akiandika "Habari za asubuhi humu, hakuna rais kilaza kama huyu wetu duniani angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala yule picha yake ukiweka ofisini nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku inakua ya mkosi mwanzo mwisho."
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: