RAIS John Magufuli amewatumia salamu wakurugenzi wote ambao ni walevi na kuwataka kuacha mara moja kabla ya kufukuzwa kazi.


Rais Magufuli alituma salamu hizo jana alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) jijini Dar es Salam.

Alisema amepata taarifa kwamba kuna baadhi ya wakurugenzi katika halmashauri ambao ni walevi na kwamba endapo hawatabadilika watafukuzwa kazi.

β€œNimepata  taarifa za watu watatu wanne hivi wakurugenzi ambao ni walevi sana. Kama uko mkurugenzi hapa na ni mlevi ni bora uache kabisa tabia za ulevi, maana tukiwagundua tutawafukuza,” alisema Rais Magufuli na kuongeza:

β€œNi lazima tujenge maadili ya nchi hatuwezi kukubali kuacha tabia hizi ziendelee.”

Pia Rais Magufuli Alisema  kumekuwapo na mgawanyiko wa makundi  kwa watumishi katika halmashauri hizo jambo linalochangia kupunguza ufanisi mzuri wa kazi, hivyo kuagiza halmashauri kumaliza makundi hayo.

β€œSisi sote tunajenga nyumba moja, lakini kwenye halmashauri kuna makundi. Unaweza kukuta kundi hili la watumishi liko upande wa wakurugenzi, lingine kwa Meya, au la chama fulani. Nawaomba  muondoe makundi na migogoro ili mfanye kazi kwa ufanisi ndio maana nimefurahi leo kuona madiwani wa vyama vingine,” alisema.

Alisema yeye adui  ni wale wanaoiibia serikali rasilimali zake, hivyo ni bora nguvu kubwa ikaelekezwa huko kupambana nao.Sambamba na hilo, aliwaomba viongozi katika halmashauri hizo kuhamasisha amani  na upendo  wa nchi ikiwamo kufanya shughuli za maendeleo na uzalendo hususani ulipaji wa kodi.

Alisema hakuna nchi duniani ambayo iliendelea bila wananchi wake kulipa kodi na kwamba atahakikisha kila fedha inayopatikana inatumika kikamilifu kwa manufaa ya Watanzania wote.

Akitolea  mfano wa madini ya Tanzanite yaliyokamatwa hivi karibuni katika  Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (NJIA), Rais Magufuli alisema siku moja walikamata almasi inayopita uwanja wa ndege ambayo walisema  ilikuwa ya  thamani ya dola za Marekani bilioni 14   lakini waliibaini ilikuwa ya tahamni ya zaidi ya dola bilioni 29.5. kwa safari moja pekee.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: