
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
NI pasua kichwa! Hatima ya mafao ya watumishi zaidi ya 9,000 walioondoshwa serikalini kwa kukutwa na vyeti ‘feki’ bado imegubikwa na kitendawili baada ya kukosekana kwa jibu la moja kwa moja hadi sasa kuwa watapata au la.
Mafao ya watumishi hao, ni pamoja na yale yatokanayo na makato ya kila mwezi kwenye mishahara yao kwa ajili ya kuchangia kwenye mifuko ya penseheni na hifadhi ya jamii ya NSSF, PSPF, GEPF, PPF na LAPF.
Watumishi 9,932 wenye vyeti feki walibainika kupitia ripoti ya uhakiki uliofanyika nchi nzima na kukabidhiwa kwa Rais John Magufuli, Aprili 28, mwaka huu.
Akizungumza na gazeti la Nipashe jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angellah Kairuki, alisema suala la mafao ya watu hao waliopoteza sifa ya kuwa watumishi wa umma baada ya kukutwa wakitumia vyeti bandia, inategemea maelekezo watakayopata baadaye, hasa baada ya utaratibu wa kuwaondoa wote kazini kukamilika.
Waziri Kairuki alisema utaratibu unaoendelea sasa ni kuhakikisha kuwa ndani ya serikali hakuna mtu mwenye cheti ‘feki’, isipokuwa hatima yao juu ya hoja ya kupata mafao au la bado halijajulikana.
“Tunachokifanya ni kuhakikisha tunawaondoa kwenye ajira watumishi wote wenye vyeti feki. Kama kutakuwa na maelekezo mengine ni baada ya mchakato huu wa kuwaondoa kukamilika,” alisema Waziri Kairuki na kuongeza: “Kwa sasa siwezi kusema watalipwa au la.”
WADANGANYIFU WALIVYONASWA
Kabla ya ripoti kukabidhiwa kwa Rais Magufuli Aprili 28, mwaka huu, mchakato wa kuwanasa watumishi hao ulifanywa na Wizara ya Utumishi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambayo ilishirikisha pia taasisi zingine za serikali ikiwamo Baraza la Taifa la Mithani (Necta).
Alipokuwa akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli, Waziri Kairuki alisema matokeo ya uhakiki yamegawanywa katika makundi manne; la kwanza likiwahusu watumishi wenye vyeti halali ambao kwa ujumla idadi yao ilikuwa sawa na asilimia 94.
Kundi la pili, kwa mujibu wa Kairuki, ndilo lililobaini watumishi 9,932 wenye vyeti vya kughushi; la tatu ni la watumishi 1,538 waliokutwa na vyeti vyenye utata ambavyo baadhi vilikutwa vikitumiwa na mtu zaidi ya mmoja na kundi la nne, lilihusisha watumishi waliowasilisha vyeti pungufu.
Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo, Rais Magufuli alimwagiza Waziri Kairuki na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, kuhakikisha watumishi hao wanaondolewa kwenye ajira haraka iwezekanavyo.
Pia alitaka wale ambao wataondoka kwa hiari yao hadi Mei 15, mwaka huu, wasishtakiwe na watakaokaidi kuondoka, wakamatwe na kufikishwa mahakamani na adhabu yao iwe kifungo cha hadi miaka saba.
Aidha, Rais Magufuli alimwagiza Waziri wa Fedha kuwaondoa watumishi hao kwenye mfumo wa malipo na aliagiza nafasi zilizoachwa na watumishi hao zitangazwe, ili zijumuishwe na 52,456 zilizotolewa katika mwaka wa fedha wa 2017/18.
Kadhalika, Rais Magufuli aliagiza watumishi waliokutwa na vyeti vya utata wasilipwe mishahara yao hadi hapo mmiliki halali atakapofahamika.
MSAKO ZAIDI
Akiwa ziarani Mkoa wa Pwani hivi karibuni, Waziri Kairuki alisema watumishi wenye vyeti feki bado wamejazana serikalini hivyo jitihada za kuwasaka hazitafikia kikomo hadi pale itakapothibitika kuwa wamemalizika na kubakia walio na vyeti halali pekee.
Alisema ingawa serikali imefanya jitihada kubwa kuwaondoa wenye vyeti vya kughushi na wanaotumia vya wenzao, lakini bado kuna watumishi wa umma wanaoendelea kutumia vyeti ambavyo si vyao na wajijue kuwa ni suala tu la muda, lakini ni lazima watakamatwa tu.
“Serikali imejitahidi sana, lakini hili zoezi lina dosari kubwa kwasababu kuna watumishi wengi ambao bado wanaendelea kutumia vyeti vya wenzao… tutaendelea kuwasaka,” alisema Kairuki, ambaye katika ziara hiyo aliagiza kusitishwa kwa mshahara wa Katibu Tawala Msaidizi Uratibu wa Serikali za Mitaa, Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani, ambaye alihakikiwa kwa cheti chenye jina tofauti na majina yanayotumika kulipwa mshahara wake.
Post A Comment: