Nahodha wa Azam FC, Himid Mao amewahakikishia mashabiki wa kikosi chake maarufu kama Wanalambalamba akisema, Simba watakayocheza nayo leo Jumamosi, haitaondoka na pointi hata moja kwenye uwanja wao wa Chamazi.


Himid ambaye ni miongoni mwa wachezaji waandamizi kikosi hapo alisema, ndani ya miaka sita ambayo wameutumia Uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex,  wamepoteza mechi nne tu.

β€œHatuna rekodi ya kupoteza mechi katika uwanja wetu ndiyo maana tulikuwa tunaomba kwa nguvu waturuhusu kuutumia kwa mechi hizo za Simba na Yanga,” alisema Himid mtoto wa kiungo wa zamani wa Pamba, Mtibwa pamoja na Taifa Stars.

Katika mechi hizo nne ambazo Azam walifungwa katika uwanja wao ni walipocheza na JKT Ruvu, Mtibwa Sugar,  African Lyon na Kagera Sugar .
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: