Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zuberi anafanya mazungumzo na waumini waliokwama kusafiri kwenda kufanya ibada ya hija Makka, Saudi Arabia.


Waumini hao takriban 100 walikwama kusafiri Agosti 23 baada ya taasisi iliyoandaa na kuratibu safari yao kuelezwa kuwafanyia udanganyifu na kuchukua fedha zao.

Kikao hicho kilichodumu kwa zaidi ya saa mbili  kikielezwa kuwa kinalenga kupata ufafanuzi wa tuhuma zinazoikabili taasisi hiyo yenye ofisi zake Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Waumini hao walisema taasisi hiyo  ilikusanya fedha takriban Sh10 milioni kutoka kwa kila muumini kwa ajili ya safari hiyo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: