ads

Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam (SACP) Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa katika kipindi chake kama kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam hakuna mtu yoyote atakamatwa kwa kauli ya 'order' kutoka juu.  


Kamanda Mambosasa amesema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kudai polisi yoyote ambaye anasema amekuja kumkamata mtu kwa 'order' kutoka juu ni wazi kuwa polisi huyo ni mbabaishaji na hajui anachotenda.

“Katika kipindi changu hutasikia kauli ya 'order' kutoka juu na ukisikia ikatie rufaa, nipigie niambie kuna mtu anataka kuchezea uhuru wangu, Ukisikia askari anasema 'order' kutoka juu ujue huyo hajiamini na pengine ni mbabaishaji hajui anachotenda" alisema Mambosasa

Aidha Kamanda Mambosasa amedai kuwa jeshi la polisi linafanyakazi kwa kuzingatia katiba, sheria na kanuni pamoja na miongozo inayoliongoza jeshi la polisi na si kitu kingine.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: