ads

MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi, amesema kwa mwenendo wa usajili wa Simba ulivyo, hakuna shaka timu hiyo ndiyo itakayochukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao wa 2017/18.


Madadi ameyasema hayo jana Ijumaa kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Kampuni ya Michezo ya Kubahatisha ya SportPesa jijini Dar es Salaam kuzungumzia ujio wa Klabu ya Everton ya England Julai 12, mwaka huu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari waliyohudhuria ndani ya semina hiyo, Madadi alisema jinsi Simba inavyoendelea na usajili wake ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu ujao.

“Simba itakuwa bingwa kwani inafanya usajili mzuri na kwa jinsi wanavyoenda ni wazi watakuwa na kikosi bora cha ushindani kwa msimu ujao wa ligi na mechi za kimataifa.

“Mabingwa wa msimu ujao Simba wanaweza kupata fursa ya kucheza na Everton pia mabingwa wetu watetezi Yanga, hii tunaomba kama itawezekana wacheze na Everton kabla ya Ligi ya England kuanza,” alisema Madadi.

Katika hali ya utani, Tarimba alijibu kijembe hicho cha Madadi kwa kusema; “Kwenye suala hili la ubingwa wa Simba msimu ujao, hebu tusubiri mwisho wa msimu tuone ila kwa kuwa amesema mkurugenzi wa ufundi haya.”
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: