BAADA ya Yanga kuondolewa katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wanatarajia kumaliza hasira zao kwenye michuano ya ndani.


Kabla ya kipigo hicho cha aibu, Yanga walipata ushindi wa bao 1-0 wakiwa nyumbani na hivyo kuhitajika kupata ushindi au sare ya aina yoyote ili kusonga mbele.

Mbali na mechi za ligi, Yanga wanarejea nchini huku wakihitaji pia kutetea kombe lao linaloandaliwa na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) maarufu Azam Sports Federation Cup ambalo tayari Azam FC, Simba  na Mbao FC wameingia hatua ya nusu fainali.

Katika mashindano hayo, Yanga wanatarajia kukutana na Tanzania Prisons Mei 6, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema timu hiyo imerejea jijini kwa mafungu ambapo kundi la kwanza liliwasili jana usiku na jingine leo mchana wakitokea Algeria.

β€œTunashukuru Mungu tumemaliza salama ingawa matokeo hayakuwa mazuri, tumewasili jana usiku na wengine watawasili leo mchana baada ya jana kulala Dubai,” alisema Hafidh.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: