
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
USHIRIKIANO wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama
vya Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Chama cha Wananchi (CUF) , NCCR
- Mageuzi na NLD, upo shakani kuendelea kudumu katika uchaguzi ujao wa
serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020, imebainika.
Dalili hizo zimeanza kuonekana kwenye kuwania nafasi za uchaguzi
mdogo wa udiwani katika Kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro,
ambavyo vyama sita ikiwemo Chadema na CUF kila kimoja kusimamisha
mgombea wake. Uchaguzi utafanyika Januari 22 mwakani.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo, Abuu Rashid Liwangile akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jana alisema wagombea wa vyama sita vya
siasa walichukua fomu na kurejesha.
Wote wamepitishwa na tayari wameanza kampeni za uchaguzi huo tangu
juzi. Alitaja vyama na wagombea waliopitishwa kuwa ni Chama Cha
Mapinduzi (CCM) mgombea wake ni Isihaka Sengo, wakati CUF mgombea wake
ni Abeid Mlapakolo.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 , Mlapakolo aliwania nafasi ya
Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini na alishindwa na mgombea wa CCM,
Abdulaziz Abood.
Mlapakolo alijaribu tena kuwania ubunge Jimbo la Kilosa kwenye
Uchaguzi Mkuu wa 2015 kupitia mwavuli wa Ukawa, lakini akawekewa mgombea
mwenza kutoka Chadema, hivyo kushindwa dhidi ya mgombea wa CCM. Mgombea
wa Chadema ni Salum Milindi, wakati TLP imemsimamisha Julius Msilanga.
Chama cha ACT- Wazalendo kimemsimamisha Rahim Elias na Sauti ya Umma (SAU) mgombea ni Mussa Kimonje.
Uchaguzi huo mdogo katika Kata ya Kiwanja cha Ndege, unafanyika baada
ya kutokea kifo cha ghalfa cha diwani wa kata hiyo kupitia CCM ,
Godfrey Mkondya, miezi michache baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana.
Mbali na Kiwanja cha Ndege, uchaguzi mdogo wa udiwani pia utafanyika
katika kata zingine 21 nchini, ambazo ni Ihumwa na Ng’ambi mkoani
Dodoma, Igombavanu na Ikweha mkoa wa Iringa, Ngarenanyuki huko Arusha,
Kijichi jijini Dar es Salaam, Kinampundu mkoani Singida, Isagehe mkoa wa
Shinyanga, Kasansa huko Katavi, Malya mkoa wa Mwanza, Maguu huko
Ruvuma.
Kata zingine ni Kimwani mkoa wa Kagera, Nkome mkoani Geita, Lembeni
mkoa wa Kilimanjaro, Duru mkoa wa Manyara, Misugusugu mkoani Pwani na
Mateves mkoa wa Arusha.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: