Rais Dkt. John Pombe Magufuli ataungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili.


Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Jumanne Novemba 28, 2017 jijini Nairobi, Kenya.

Katika hatua nyingine Rais Uhuru Kenyatta amemwalika mshindani wake mkuu ambaye ni kiongozi wa NASA Raila Odinga kuhudhuria katika sherehe hizo zilizopangwa kufanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani.

 Katika orodha ya baadhi ya wageni waalikwa wamo Cyrus Jirongo (Joseph Momanyi); Michael Wainaina (Miriam Mutua) na Odinga na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: