MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) jana alihojiwa na Polisi jijini Dar es Salaam kwa saa sita, kuhusu mkutano wake na wanahabari wiki iliyopita kuzungumzia kupotea kwa Ben Saanane.


Saanane ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Sera wa Chadema na msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na ilielezwa alipotea tangu Novemba 14 mwaka huu na mpaka sasa haijajulikani alipo.

Akizungumza jana, Lissu alisema hakukamatwa, bali aliitwa kuhojiwa kuhusu mkutano wake na wanahabari wiki iliyopita.

“Sijakamatwa ila nimeitwa kuhojiwa kuhusu ile ‘Press Conference’ (mkutano na waandishi wa habari) ya wiki iliyopita na nimetakiwa nitoe maelezo kuhusu Saanane. “Nilitakiwa nifike polisi saa mbili asubuhi kituo cha kati (kituo kikuu). 

Nimefika saa nne kuhojiwa kuhusu mambo mawili; moja nitoe ushahidi kuhusu kupotea kwa Ben Saanane na kauli zilizoitwa za uchochezi nilizozitoa katika mkutano wangu na waandishi wa habari,” alisema Lissu aliyehojiwa hadi saa kumi jioni.

Hivi karibuni, Lissu alisema Chadema haifahamu alipo Saanane na kuitaka serikali ieleze mahali alipo msaidizi huyo wa Mbowe kwa kuwa moja ya kazi za chombo hicho ni kulinda raia wake.

Hata hivyo, juzi Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Boaz, alisema Polisi haijui alipo Saanane na inaendelea na uchunguzi wa kina kubaini alipo kiongozi huyo wa Chadema.

Aidha, alieleza kuendelea na uchunguzi wa miili saba iliyokutwa kando ya Mto Ruvu wilayani Bagamoyo ikiwa imefungwa katika mifuko ya sarandusi.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: