
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
KAMPUNI ya Kupakua na Kusafirisha mizigo ya ABG African Link iliyopo
Buguruni Sukita, Dar es Salaam imeamriwa kuhama katika eneo walilopewa
na Kampuni ya Jitegemee Trading Company inayomilikiwa na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kushindwa kulipa kodi ya pango ya Sh
bilioni 1.3.
Aidha, Kampuni ya Udalali ya Yono, jana ilianza kutoa vitu mbalimbali
vilivyokuwepo kwenye majengo ya kampuni hiyo baada ya notisi ya saa 24
waliyopewa kumalizika.
Mwenyekiti wa Kampuni hiyo ya udalali, Stanley Kevela alisema kuwa walitoa notisi kuitaka kampuni hiyo kuhama eneo
hilo tangu Jumanne ambayo iliisha juzi.
Alisema Yono itaendelea kufuatilia deni hilo la kodi hadi
litakapolipwa vinginevyo, itafuatilia mali na kuzikamata kwa ajili ya
kuzipiga mnada.
“Watu wameona mali za chama kuwa ni sehemu ya kujineemesha, nasi kama
kampuni tuna uchungu na chama, hivyo tutahakikisha fedha hizo
zinapatikana na tutatafuta mtu anayestahili atakayewekeza katika eneo
hilo,” alisema Kevela.
Akielezea tukio hilo, Meneja Uendeshaji wa kampuni ya ABG, Mmad
Abubakar alisema si kweli kwamba wanadaiwa kodi hiyo, bali ni mgogoro wa
kisheria kati yao na Jitegemee ambao waliingia mkataba tangu 2008.
Alisema walipewa eneo hilo la Sukita wakati huo likiwa shamba na
lengo ni kuliendeleza na kwamba walipewa mkataba wa kukaa bure kwa miaka
mitatu.
“Baada ya kupewa shamba tuliwaambia wabadilishe hati iwe ya biashara
ambapo ilikuwa na namba 1010 iliyopatikana 2012 ndipo tukaanza ujenzi na
muda wa kukaa bure umeisha 2015 ambapo tulikabidhiwa eneo lenye urefu
wa meta za mraba 50,000,’’ alisema.
Alifafanua mwaka 2014, Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) iliwapa barua kuuondoa ukuta uliokuwa pembezoni mwa mto Msimbazi
na kujenga meta 60 kuingia ndani, hivyo kubakiwa na eneo la meta za
mraba 12,000 kati ya meta za mraba 50,000 na kwamba kinachogombaniwa ni
nani atagharamia ujenzi wa ukuta huo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: