Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ndiyo timu iliyotangaza rasmi kutaka kumnasa mshambuliaji Thomas Ulimwengu.

Ulimwengu ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na TP Mazembe, ameanza mazunguko na Genk ambayo anaichezea Mbwana Samatta.

Habari za uhakika, zimeeleza kuwa, Ulimwengu amekubali kujiunga na Genk licha ya ofa zaidi ya 10 kuwa mezani, lakini analazimika kusubiri.

“Analazimika kusubiri kidogo hadi wakati wa dirisha dogo wakati Genk watakapomuuza yule beki wao wa kati (Ndidi) raia wa Nigeria, anakwenda Leicester City kwa dau la pauni milioni 15,” kilileza chanzo kutoka nchini Ubelgiji.

Pamoja na Genk, taarifa zilieleza kuwa kuna timu nyingine mbili za Ubelgiji zimeonyesha kumtaka Ulimwengu lakini bado ni suala la makubaliano tu.

Alipoulizwa Meneja wa Ulimwengu, Jamal Kisongo kuhusiana na suala hilo, alisema: 
 
“Ulimwengu anatakiwa na zaidi ya timu kumi, kama mwanzo nilieleza tuko kwenye mazungumzo,” alisema Kisongo.

“Genk ni moja wapo, lakini kuna Oostende, pia kuna klabu kubwa kama Anderlecht. Lakini ni suala la kusubiri kwanza. Mambo yakiwa tayari, muwe na subira, tutawaeleza.” 


Ulimwengu ambaye alifanikiwa kubeba ubingwa wa Afrika akiwa na TP Mazembe, amekuwa na soko kubwa kutokana na mambo mawili. Moja ni mafanikio yake uwanjani na timu hiyo ya DR Congo, lakini kuwa mchezaji huru, pia inaonekana kuzivutia timu nyingi za barani Afrika na zile za Ulaya.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: